Pages

Wednesday, 7 November 2012

VIOLENCE AGAINST WOMEN



Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina  la Henry amejikuta mikononi mwa vyombo vya dola baada ya  kumchoma mkewe  sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia  pasi na kumuua mtoto wake  wa  mwaka  mmoja kwa madai kuwa mwanamk huyo amekuwa akitoka kmaenzi na baba yake mzazi........
Akiongea kwa majuto makali huku akiwa "nyuma ya nondo", Henry anadai kuwa alifanya hivyo bila kukusudia
"Nakiri kwamba nilifanya maamuzi ambayo sikutegemea kuyafanya katika maisha yangu.Nilikuwa napandwa na hasira  kubwa kila nikimuona yule mtoto akiamka na kulilia maziwa .
Moyo ulikuwa ukijaa nakunifanya nishindwe  hata kupumua  na ndipo  siku moja ndani ya moyo wangu nilisikia sauti ikiniamuru  nimuue yule mtoto maana  si damu yangu. 

Bila kujizuia, nilimshika shingoni, nikamkaba na kumpiga  kwa nguvu......." Henry alielezea tukio hilo huku aimwaga machozi  ya uchungu
"Najua kuanzia  sasa maisha yangu  yatakuwa  ni gerezani tu.Nakubaliana na yote  ila  nimeona  ni bora jamii  iujue ukweli.......

Mke wangu Mercy alikuwa na mahusiano  ya  kimapenzi na baba yangu mzazi .Kabla ya tukio hili, nimekuwa  nikimuonya mara nyingi sana kwamba  aache tabia hiyo na  asiende nyumbani kwa baba  maana nilikuwa nimeshausoma  mchezo huo.Mbaya zaidi mke wangu hakutaka  kunisikiliza.....

Siku moja mke wangu aliaga kuwa  anataka kwenda kwa rafiki yake.Nilimkataza na  kumwambia kuwa asitoke  wala kwenda kokote  lakini  hakunisikia.Baada ya muda kidogo nilizuga  na kumwambia kuwa natoka kidogo.Baada ya nusu saa nilirudi  nyumbani na sikumkuta mke wangu.....
....Nilisubiri kidogo huku akili ikiwa haifanyi kazi.Baadaye moyo ulinituma kuwa niende  kwa baba nikamuangalie maana si mbali sana kutoka nyumbani........

Nilifika na kugonga mlango.Baba alitoka akiwa amejifunga taulo tu.Nilipojaribu  kuingia ndani alinizuia.Baada  ya kuzozana  naye kwa muda  niliamua kuacha  na kurudi nyumbani.......Sijui mke wangu alitorokaje  na kuniwahi kufika  nyumbani, lakini niliporudi nilimkuta ameshafika.

Badala ya  kuchukia, nilijiuta nacheka sana .yaani nilikuwa kama mtu aliyerukwa na akili.Nilijisogeza  pembeni  na kuanza  kuvuta sigara ili kupunguza hasira......
Ilipofika usiku, nilichukua nguo yamteja wangu na kuanza kuipiga pasihuku nikiwa na mawazo mengi.Baadae nilisikia sauti ndani ya  moyo wangu ikiniambia  nijikaze japo nimulize ili niujue ukweli.Wakati huo pasi ilikuwa  ni ya  moto kwelikweli. Ghafla maamuzi yakaniijia kuwa niitumie ile pasi kumtisha ili aniambie ukweli wa tukio zima......
Nilimsogelea na kumwamsha.Alipoamka  nilimuomba anieleze ukweli  tena  kwa  nia  nzuri kabisa.Mercy hakunijibu  kitu  na badala yake alikaa kimya.Nilijawa  na hasira  na kujikuta  namchoma  kwa  kutumia ile pasi
Nilipofanya vile,Mercy alikiri kuwa  amewahi  tembea  na  baba yangu mara  tatu.....Aliposema vile hasira zilinipanda zaidi na  kujikuta namchoma zaidi......
Wakati nafanya vile,mtoto aliamka na kuanza  kulia kama ishara  ya  kutaka kunyonya.Nilimwangalia kwa hasira  huku moyo ukiniambia  kuwa yule  si mwanangu...."
Henry alikaa  kimya kwa  muda huku  akiwa amejiinamia.Baada ya muda  kidogo  alinyanyua kichwa  na kuangalia  juu  huku  uso wake ukiwa umelowa machozi....
Baada ya kimya cha muda, Henry  aliendelea kwa kusema  kuwa:"Yalikuwa  ni  maamuzi mabaya  sana.Wakati yule mtoto akilia, nilimshika na  kumkaba shingo.Baada ya kumkaba  nilimpiga  kwa ngumi.
Wakati najiandaa kumpiga mara ya pili, mke wangu aliudaka mkono wangu.Nilipoona ameshika mkono, nilitumia mkono mwingine kumuunguza zaidi  huku  mkono mwingine ukiendelea kumpiga  mwanangu.....Mwanangu  hakuweza kutoa sauti tena."Alimalizia Henry huku akilia kwa sauti kubwa 

No comments:

Post a Comment