We are UNITED against tribalism in KENYA. lets PREACH peace
Pages
▼
Sunday, 6 January 2013
JOSHUA WAIGANJO SAGA IN KISWAHILI
HABARI ZA DHARURA KUTOKA KWA DAKTARI JARUNDA
Aliajiriwa na Iteere; Familia ya 'PPO' yadai Familia ya Joshua Waiganjo, mshukiwa anayezuiliwa na polisi kwa kudai kuwa naibu PPO mkoani Rift Valley, imedai kwamba mwanao aliajiriwa na Kamishna wa polisi kuwa polisi wa akiba na baadaye kupandishwa cheo kwa haraka. Babake mshukiwa huyo Ibrahim Waiganjo ambaye ni afisa mustaafu wa polisi na sasa ni mhubiri amesema kwamba mwanaye amekuwa akiihudumia idara ya polisi kwenye wadhifa wa polisi wa akiba kwa muda. Amesema aliachishwa kazi wakati wa muhula wa Kamishna Hussein Ali lakini alipokuja Mathew Iteere, alimwajiri tena kwenye huduma iyo hiyo ya polisi wa akiba. Amesema ni wakati huo ndipo alipandishwa cheo kufikia naibu mkuu wa polisi mkoani. Waiganjo amesema hayo kwenye kikao na wanahabari nyumbani kwake Njoro ambapo pia ametoa picha zinazoonyesha baadhi ya wakuu wa polisi wakiwa na mwanaye
No comments:
Post a Comment