Pages

Thursday, 28 March 2013

TESO NEWS

TESO: Ushirikina

Wakaazi wa eneo la Teso kaskazini katika kaunti ya Busia wameonywa kukoma kuchukuwa sheria mikononi mwao dhidi ya watu wanaoshukiwa kuwa wachawi.

Mkuu wa polisi wa Teso Elphas Korir ameonya kuwa hatasita kumchukulia hatua kali mtu yeyote ambaye atajaribu kuadhibu washukiwa wa ushirikina katika eneo hilo.

Korir alikuwa akiguzia kisa cha hapo jana ambapo wananchi waliokuwa na ghadhabu walivamia boma la mama mmoja mzee na kuteketeza nyumba yake wakidai kuwa alisababisha kifo cha mkaazi mmoja wa kijiji hicho.

Mkaazi huyo alifariki akipokea matibabu katika hospitali kuu ya Bungoma aliko kimbizwa baada ya kuangukiwa na mti aliokuwa anataka, huku wenyeji wakishuku kuwa alifanyiwa mazingaumbwe na ajuza huyo.

Kwa sasa polisi wanawasaka wale waliohusika kuchoma nyumba ya mama huyo ambapo Korir ameahidi kuwatia mbaroni na kuwafungulia mashtaka.

Hata hivyo, baadhi ya wenyeji wa eneo hilo wamewalaumu maafisa wa polisi kwa kutochukua hatua za haraka na kuzuia mashambulizi dhidi ya ajuza huyo.

* * * * * *

No comments:

Post a Comment