Tuesday, 26 March 2013

Utakuta kabinti kazuri zuri tu kadogo kadogo kamevunja ungo wa kwao miaka kadhaa iliyopita hata harufu ya maziwa bado
haijatoka vzuri ila ana msururu wa mabwana mpaka unamuogopa ukionyeshwa watu
anaomka nao unaweza kutaka kupiga simu usalama wa taifa wampe ulinzi madhubuti.

Kanasoma shule ya kata huko ana bwana wake mwanafunzi mwenzie ambae ndio anagharamia mambo ya chips yai shule daily anamkamua mtoto wa mwanamke mwenzie japo anajua hana kazi na ni mwanafunzi
kama yeye.

Usije kushangaa yule mwalimu wa english au math ni bwana wake anaem-save kama akifanya soo shule huyo ndio huwa
anamtetea asichapwe au kupewa suspension.

Njiani kuna jamaa muuza chips au muuza duka nae anakula mambo yake huyu ndio anamfanya atambe shida zake msosi kama
nyumbani wakipika ugali zinamalizwa na huyu bwana.

Alafu mtaani kuna kisharobaro chake huyu ni wa kuuzia sura kwenye sherehe au cku wakienda coco beach anaenda nae huyu
hana kitu ila anampenda kwa kuwa ni msafi anajua kupiga pamba.

Alafu kuna baba Juma mwenye mke na watoto kadhaa huyu ndie kachukua nafac ya baba yake kuanzia ada ya shule,nauli na hela
ya kutumia bila kusahau nguo za ckukuu.

Huyu ndie baadae anamaliza form 4 anapata buyu anailaumu serikali alafu maisha yanaendelea sasa akishamaliza shule ndio Mungu wangu fungulia mbwa mpaka
anafikisha miaka 25 hao watu aliowahi kudate nao unaweza kuwapanga kutoka ubungo mpaka kwenye pantoni kule ferry.

Huyu ndio anakuja kuwa mama mwenye familia yake ebu jiulize huyo binti yake atakuaje anaweza hata kumshauri asome na aachane na anasa za wanaume wa mjini?

No comments:

Post a Comment